NIKI A PILI

Nikki wa Pili ampongeza Rais Magufuli

Fadhil Kayanda · 1 hour ago

Msanii wa Nikki wa Pili, amempongeza Rais Magufuli kwa kitendo alichokifanya leo cha kumtumbua Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo na kumwambia Mungu amsimamie katika kupambana na ufisadi. 

Niki ametoa salamu hizo za pongezi kupitia ukurasa wake wa kijamii instagram kwa kusema watanzania wanaopewa dhamana wasipoamua kuwa waadilifu umaskini utaweza kuandika historia tukufu kwa Tanzania. 

“Wizi mkubwa utamkuta mwekezaji na wakala wake wa kitanzania (wasomi, viongozi, wafanya biashara) yaani ni kama ule uchumi wa kikoloni manufaa ni kwa kampuni ya nje na kitabaka cha watanzania wachache…Nimpongeze Mkuu wa nchi kwa kuamua kupambana na ufisadi huu…Ila vita ya kuvunja mfumo wa kiuchumi wa kifisadi ni hatari…Kina Lumumba, Sankara huko Chile, Nikaragwa, Venezuela, Haiti, Iran…Viongozi hawakupona ni vita kuu Mungu akusimamie”. Ameandika Nikki wa Pili. 

Advertisements

Utenguzi wa waziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia leo tarehe 24 Mei, 2017.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Sa

NJIA ZA KUONDOA HOFU YA FANIKIO

FB_IMG_1492314293387Tumia njia hizo ili kuondokana na hofu ambayo imejengeka ndani mwako kwani hofu ni adui namba moja wa maisha yako ya mafanikio kama utaendelea kuibeba.
 
1. Muombe  mwenyezi Mungu.
Kila wakati na  kila siku hakikisha unamuomba Mwenyezi Mungu akusaidie kuweza kuondokana na hofu kubwa ambayo imekuwa ikijengeka ndani yako. Haijalishi ni imani gani uliyonayo ila hakikisha unamuomba Mungu akusaidie juu ya hilo.
2. Acha kujilinganisha na wengine.
Mafanikio ni haki yako, kila wakati hivyo kama unaamini juu ya hili, unachotakiwa kufanya ni kuweza kusimama wewe kama wewe katila jambo lako ulifanyalo, watu wengi tunashindwa kufanikiwa kwa sababu tunataka kujifananinisha na wengine. Na athari kubwa ambayo ambayo itatokea pale unapotaka kujifananisha na wengine ni kwamba utajiona huwezi kufanikiwa.
Nb; hivyo wewe ni mwenye mafaniko kuanzia sasa, endapo utaacha mara moja kujilinganisha na wengine.
3. Chukua hatua ya kuendelea mbele kivitendo.
Tumia njia hii katika kusonga mbele, acha maneno weka vitend. Watu wengi tumejenga maneno mbele kuliko vitendo na hii hofu kubwa imejengeka sana miongoni mwa watu, hivyo ukijijengea uwezo wa kivitendo zaidi utakufanya uondakane na hofu iliyopo ndani yako.
Inawezekana kabisa labda ukawa tayari umeshanza kufanya vitu fulani ila huna imani ya kufanikiwa zaidi, ninachoweza kukwambia ni kwamba, siri ya mafanikio yako inatokana na vile ambavyo unaamini, hivyo kuanzia sasa anza kuwaza chanya dhidi ya kile ukifanyacho, kwani kama endapo ukiamini, utaenda kufanya jambo hilo kwa nguvu na bidii na kuleta matokeo chanya.
4. Acha kuangalia tatizo kama tatizo, bali tafuta majibu ya tatizo husika.
Moja ya matatizo/ changamoto ambazo zinatokea katika jamii ni chanzo kikubwa cha kuleta hofu ya mafanikio. Kwa mfano mtu anafanya biashara fulani ila baada ya muda fulani kuna changamoto inajitokeza katika biashara hiyo, utashangaa muda fulani mtu uyo anaacha kufanya jambo hilo nakufanya jingine.
Hivyo ili kuishinda hofu iliyomo ndani yako unachotakiwa kufanya, ni kuhakikisha kila changamoto inayojitokeza ni sehemu mafanikio na sio sehemu ya kushindwa.
Kwani kuna mwandishi fulani, aliwahi sema ” fear is danger, success is real.
5. Baki na mawazo chanya kila wakati.
Mara nyingi hofu  zimekuwa zikitawala katika mioyo na fikra zetu, hii ni kutokana na mawazo hasi tuliyoyabeba, kwa mfano watu wengi wanaamini ya kwamba wao kufaulu katika mtihani wa kutoka hali ya umaskini ni suala gumu sana.
Lakini ukweli n kwamba kama kweli unataka kufanikiwa katika jambo ambalo unataka kulifanya hakikisha ya kwamba unawaza chanya juu ya jambo, kwani kuna usemi usemao uwazo mtu ndivyo atakavyokuwa, hivyo anza kuwaza chanya kwa kila jambo kuanzia sasa, kwani kufanya hivyo ni njia tosha ya ulekeo wa mafanikio yako.
6. Anza na kidogo ulichonacho.
Njia moja wapo ya kuendelea kusonga mbele na kuagana na woga ni ile hali ya kuanza na kile ulinaonacho, kwani aliyenacho huongezewa. Usisubiri mpaka ufikishe kiasi fulani cha fedha ndo uanze jambo hilo, kwani haba na haba hujaza kibaba na ngoja ngoja yaumiza matumbo.
mpaka ufikishe kiasi fulani ndo uanzishe jambo lako, ila jambo la msingi ni kuhakikisha kwa kile kidogo ulichonacho kumbuka kuanza kukifanyia kazi huku ni nidhamu ya muda na fedha ikipita mkondo wake.
 

 

7. Fanya kitu unachokiogopa.
Haua ya sita ni kwamba, njia bora ya kuondokana na hofu ni kufanya kile kitu ambacho unakiogopa. Kwa mfano kama ulikuwa unaogopa kufanya biashara fulani anza kufanya sasa, kama ulikuwa unaogopa kuonesha kipaji chako anza sasa. Usitake kuendelea kuangalia nani atasema nini bali simama wewe kama wewe huku, ukisonga mbele kila wakati.

SOLUTION TO PROBLEMS.

20170506_160042Je wewe ni miongoni mwa watu ambao hukata tamaa katika maisha? Kama jibu ni ndiyo makala hii inakuhusu sana, cha msingi nakusihi usome makala haya mwanzo hadi mwisho.

Miasha ya mwanadamu yamejawa na changamoto na shida mbalimbali. Changamoto hizo hizo, wapo baadhi ya watu huzivumilia katika kutenda jambo fulani, lakini pia wapo baadhi ya watu hukta tamaa kabisa. Na hao ambao hukata tamaa ndio ile idadi kubwa ya watu ambao hufa ni ndoto zao mapema.

Lakini ukweli ni kwamba changamoto na shinda mbalimbali za maisha ni kipimo cha akili, kwani wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo huimba katika nyimbo zao na kusema changamoto ni majaribu, na majribu ni mtaji. Hivyo katika maisha haya ni jambo la ajabu sana kama utaendelea kukataa tamaa katika maisha yako kwani hakuna dhambi kubwa kama kukata tamaa.

Na ukweli ni kwamba ili uweze kufanikiwa wanasema changamoto hazikwepeki, na changamoto ndio njia ambayo itakufikisha kule ambapo unataka kufika, endapo tu utaamua kupambana na changamoto hizo.

Swali linakuja nawezaje kupambana na changamoto hizo?

Jambo la msingi unalotakiwa kufanya ni kuhakikisha unapambana na changamoto za maisha ni;

Orodhesha changamoto zote ambazo zinakukubali. Hata kama zipo zaidi ya changamoto tano ainishea zote.

Baada ya kuorodhesha changamoto hizo tano, jambo ambalo unatakiwa kufanya baada ya hapo unatakiwa kuchugua jambo ambalo lina umuhimu sana katika kulitekeleza.

Baada ya kulipata jambo hilo, usiishie kulichagua tu. Tafuta mbinu ya jinsi ya kuondokana na changamoto hiyo. Na mbinu hizo ziandikwe mahali ambapo panaonekana na uanze utekelezaji mara moja.

Mbinu hii ya kupambana na changamoto itakusaidia sana katika kupiga hatua mbele zaidi kivitendo kuliko kukata tamaa.
Nimekupa mbinu hii, kwa sababu wengi wengi huwa tunajitenga na chanagamoto za kimasha hasa pae zinapojitokeza. Lakini kama nilivyoeleza hapo awali ni kwamba changamoto za kimaisha ni kigezo tosha cha kuweza kutimiza ndoto yako, jambo la msingi tafuta majibu ya jinsi ya kuondokana na changamoto hiyo.

Kama hutatafuta majibu ya changamoto zinazokukabli itakuwa ni sawa na bure, kwani utazidi kuwa maskini maisha yako yote.

WAZIRI MKUU ANUNUA HISA VODACOM

 


Alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mbele ya wakuu wa masoko ya Hisa na Dhamana, Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na Kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kueleza alichofanya, Waziri Mkuu aliwasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao.

Alisema anajua watumishi wa umma wamepewa fursa ya kununua hisa hizo kupitia mipango iliyowekwa na Makatibu Wakuu wao, lakini pia amewasihi viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi wachangamkie fursa hiyo ili nchi iweze kupata kodi kupitia makampuni hayo.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema uwekezaji kwenye hisa ni njia mojawapo ya kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi.

Alisema sekta ya mawasiliano ni miongoni mwa sekta inayokua kwa kasi hapa nchini kwani katika robo tatu ya mwaka, sekta hiyo imekua kwa asilimia 11.3 na kuwasihi watanzania kununua hisa za Vodacom ili waweze kuboresha uchumi.

Waziri Mpango alisema anatoa ombi maalumu kwa wafugaji kukubali kuuza mifugo yao na kununua hisa ili kupunguza idadi ya mifugo yao na kupunguza misuguano baina yao na wakulima.

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana, Nassama Masinda alisema amefurahishwa kuona Waziri Mkuu akinunua hisa za kampuni ya Vodacom katika soko la awali.

Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao alisema mauzo ya hisa yanayofanywa na kampuni hiyo ni makubwa mara nne ya mauzo ambayo yamewahi kufanyika hapa nchini. Alisema kampuni hiyo ambayo imekwishafanya kazi kwa miaka 17 hapa nchini, imewekeza zaidi ya Sh trilioni mbili katika mtandao wa mawasiliano nchini Tanzania.

TABIA ZA kijanja

20170420_213150-1POLISI mkoani Mwanza inamshikilia mtu mmoja nayejulikana kwa jina la Mkama Mgengele (36), mkazi wa kisiwa cha Ghana katika Kijiji cha Kamasi Kata Ilangala wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, kwa tuhuma za  kumfanyia ukatili mtu anayedaiwa kuwa mpenzi wake kwa kumkata kiganja cha mkono wake wa kushoto.

Mgengele anadaiwa kufanya tukio hilo la kumkata na kitu chenye ncha kali kwenye kiganja cha mkono wa kushoto hadi kudondoka chini mpnzi wake huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi,  alisema Mei 14 mwaka huu majira ya usiku, mtuhumiwa alimkata kiganja cha mkono wa kushoto kisha akamkata tena kwenye paja la mguu wa kulia, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Ester Lazalo (37)ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake.

Msangi alikuwa hivi karibuni walikuwa katika mgogoro wa kimapenzi na kwamba mtuhumiwa alifika kazini kwa Ester na kuanza kumrushia maneno makali kabla ya kumkata.i kuimba kwenye wimbo huku akiuliza serikali ni nini? Maana imekukuwa ikutupiwa lawama kwa kila kitu. Ndugu msomaji wa makala haya nakusihi na kukushauri pia kwa kile ambacho unaweza kukifanya usisubiri serikali ndio ukifanyie, kama unauwezo wa kufanya usafi katika eneo lako fanya usisubiri kuambiwa, maana tabia za bianadamu kwa asilimia kubwa wanasubiri kuambiwa fanya hiki fanya kile . UKisubiri kuambiwa maisha ya mafanikio kwa upande wako yatakuja kwa asilimia chache sana.

Kitu cha msingi ya kuzingatia ni kwamba tuache lawama sizisokuwa na msingi wowote, kwani lawama ulizonazo leo hata yule unayemlalamikia hakusikii na unazidi kuwa maskini tu. Jambo la msingi fanya kila kitu kwa moyo mmoja bila kusubiri mtu fulani akwambie ufanye. Daima tukumbuke usemi huu “ kila uonapo nyundo usifikiri kila tatizo ni msumari’’

Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kujitambua yeye ni nani? Na ni kwanini upo hapo ulipo. Kuna usemi mmoja hivi wa kiswahili unasema kila binadamu ni mchungaji ,kama ndivo hivyo basi kama mimi leo nikiulizwa nimechunga nini, jibu langu litakuwa lipo wazi ya kwamba natumia muda mwingi kuwafunza watu ili kujua mbinu za kufanikiwa, je wewe mwenzangu unasoma makala hii endapo utaulizwa swali kama hilo utajibu nini? Tafakari kisha uone una thamani gani mbele ya watu wengine?

Tunakutakia mafanikio mema na kila kheri katika harakati za kuboresha maisha yako.
Kwa makala nyingine nzuri za mafanikio na maisha endellea kutembelea Blog yangu kwa kujifunza zaidi. https://mapesasite.wordpress.com