WAZIRI MKUU ANUNUA HISA VODACOM

 


Alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mbele ya wakuu wa masoko ya Hisa na Dhamana, Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na Kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kueleza alichofanya, Waziri Mkuu aliwasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao.

Alisema anajua watumishi wa umma wamepewa fursa ya kununua hisa hizo kupitia mipango iliyowekwa na Makatibu Wakuu wao, lakini pia amewasihi viongozi mbalimbali wa Serikali na taasisi wachangamkie fursa hiyo ili nchi iweze kupata kodi kupitia makampuni hayo.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema uwekezaji kwenye hisa ni njia mojawapo ya kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi.

Alisema sekta ya mawasiliano ni miongoni mwa sekta inayokua kwa kasi hapa nchini kwani katika robo tatu ya mwaka, sekta hiyo imekua kwa asilimia 11.3 na kuwasihi watanzania kununua hisa za Vodacom ili waweze kuboresha uchumi.

Waziri Mpango alisema anatoa ombi maalumu kwa wafugaji kukubali kuuza mifugo yao na kununua hisa ili kupunguza idadi ya mifugo yao na kupunguza misuguano baina yao na wakulima.

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana, Nassama Masinda alisema amefurahishwa kuona Waziri Mkuu akinunua hisa za kampuni ya Vodacom katika soko la awali.

Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao alisema mauzo ya hisa yanayofanywa na kampuni hiyo ni makubwa mara nne ya mauzo ambayo yamewahi kufanyika hapa nchini. Alisema kampuni hiyo ambayo imekwishafanya kazi kwa miaka 17 hapa nchini, imewekeza zaidi ya Sh trilioni mbili katika mtandao wa mawasiliano nchini Tanzania.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s